Psalms 9

Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Haki Yake

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa muth-labeni.
Muth-labeni ni mtajo mmojawapo katika lugha za muziki.
Zaburi ya Daudi.

1 bEe Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote,
nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.
2 cNitafurahi na kushangilia ndani yako.
Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.

3Adui zangu wamerudi nyuma,
wamejikwaa na kuangamia mbele zako.
4 dKwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu;
umeketi kwenye kiti chako cha enzi,
ukihukumu kwa haki.
5 eUmekemea mataifa na kuwaangamiza waovu;
umeyafuta majina yao milele na milele.
6 fUharibifu usiokoma umempata adui,
umeingʼoa miji yao;
hata kumbukumbu lao limetoweka.

7 g Bwana anatawala milele,
ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.
8 h iMungu atahukumu ulimwengu kwa haki,
atatawala mataifa kwa haki.
9 Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa,
ni ngome imara wakati wa shida.
10 jWote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,
kwa maana wewe Bwana,
hujawaacha kamwe wakutafutao.

11 kMwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni,
tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.
12 lKwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka,
hapuuzi kilio cha wanaoonewa.

13 mEe Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa!
Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,
14 nili niweze kutangaza sifa zako
katika malango ya Binti Sayuni
na huko niushangilie wokovu wako.
15 oMataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba,
miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha.
16 p Bwana anajulikana kwa haki yake,
waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.

17 qWaovu wataishia kuzimu,
naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
18 rLakini mhitaji hatasahaulika siku zote,
wala matumaini ya walioonewa hayatapotea.

19 sEe Bwana, inuka, usimwache binadamu ashinde.
Mataifa na yahukumiwe mbele zako.
20 tEe Bwana, wapige kwa hofu,
mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.
Copyright information for SwhNEN